Neema Gospel Choir Yatoa Msaada wa Bajaj kwa Kituo cha Watoto yatima Cha Real Life International Ministries

Neema Gospel Choir imetoa msaada wa bajaj leo kwa Makao ya Watoto ya Real Life, yaliyopo Buza, Temeke, Dar es Salaam. Msaada huu wa hisani ni sehemu ya mpango endelevu uitwao, “INSPIRE, EMPOWER, TRANSFORM – For The Better World,” wenye lengo la kusaidia Watoto Yatima na kuboresha maisha yao.

Bajaj hii itatumika kama chanzo muhimu cha mapato kwa kituo hiki cha watoto yatima kama chazo cha mapato, ikisaidia usafiri kwa watoto waendapo shule na kukidhi mahitaji ya elimu na muhimu kwa watoto. Sehemu ya mapato yatakayopatikana kutokana na uendeshaji wa bajaj hii yatawekwa katika akaunti ya UTT Amis kwa ajili ya malenho endelevu, kuwa na msaada wa muda mrefu kwa watoto hao.

Tukio la leo limehusisha kukabidhi rasmi bajaj na shughuli mbalimbali za kuvutia na watoto na walezi wao. Jitihada hii inaonyesha dhamira ya pamoja ya Neema Gospel Choir na Real Life International Ministries ya kuinua na kuwawezesha watoto katika jamii yetu.

“Tunajivunia sana kuunga mkono Real Life International Ministries katika maono yao ya kipekee,” alisema Samuel Nkola Mwenyekiti wa Neema Gospel Choir. “Msaada huu ni ushahidi wa kujitolea kwetu kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya watoto. Kupitia mpango wetu endelevu wa, ‘INSPIRE, EMPOWER, TRANSFORM,’ tunalenga kuunda dunia bora kwa vizazi vijavyo.”

Real Life International Ministries wameeleza shukrani zao za dhati kwa msaada huu wa ukarimu. Msaada wa bajaj unakuwa mwanzo wa ushirikiano wa matumaini wenye lengo la kuboresha ubora wa maisha ya watoto na kupanua huduma zao.

Kwa maelezo zaidi na kujumuika katika program hii tafadhali wasiliana na: [email protected]

Facebook
Twitter
LinkedIn
Pinterest

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Recent Posts